MWANZA PRESS CLUB

Home

Leadership

Noticeboard

Activities

Membership

Achievements

Constitution

Photo gallery

Links

 

MPC - NOTICE BOARD

TANGAZO LA UTARATIBU MPYA WA KUPATA VIWANJA


Ufuatao Ndio Utaratibu Mpya Wa Kupata Viwanja Toka Halmashauri Ya Jiji:
1. Maeneo Yafuatayo Yapo Tayari Kwa Ajili Ya Kugawia Watu Viwanja.
a) Buswelu
b) Nyegezi

2. Utaratibu Utakaotumika Kugawa Viwanja Hivyo Kuanzia Jumatatu Tarehe 14/3/2005 Ni Kama Ifuatavyo:

a) Utatolewa Muda Wa Wiki 2 Ambapo Wale Waliochangia
Gharama Za Upimaji Watapewa Nafasi Ya Kuchagua Na
Kulipia Viwanja Wanavyovitaka.

b) Baada Ya Muda Huo Kupita Viwanja Hivyo Vitatangazwa Kwa Umma Ili Mtu Yoyote Aweze
Kununua. Bei Ya Viwanja Hivyo Ni Kama Ifuatavyo:

Buswelu
High Density 360,000/=
Medium Density 640,000/=
Low Density 720,000/=
Bb 5,500,000/=

Nyegezi
High Density 450,000/=
Medium Density 800,000/=
Low Density 1,200,000/=
Bb 7,700,000/=

Kwa Yule Aliyechangia Gharama Za Upimaji Atalipia Tofauti Kati Ya Fedha Alizochangia Na Bei Ya Kiwanja Anachotaka. Hivyo Kwa Anayetaka Anakwenda Jiji Ananunua Fomu Sh. 5000/=, Anachagua Kiwanja Anachotaka Na Kulipa Zaida Ya Nusu Ya Thamani Ya Kiwanja Zinazobaki Analipa Katika Kipindi Cha Miezi 2.


c) Kwa Yule Aliyechangia Akishindwa Kulipia Gharama Hizo Atarudishiwa Fedha Alizochangia Mara Moja.

Gharama Hizo Mpya Ni Kulipia Fidia Ya Viwanja Kwa Mujibu Wa Sheria Za Ardhi, Na Uwekaji Wa Miundo Mbinu Kwenye Maeneo Hayo.

Abubakar Karsan
Mwenyekiti MPC


[Home] [Leaders] [Noticeboard] [Activities] [Membership] [Achievements] [Constitution ][Photos] [News] [Links]

MWANZA

Mazingira

Newsletter

TAA Newspaper

Mwanza Community